Nav bar

Jumatatu, 28 Oktoba 2019

MAWAZIRI AFRIKA MASHARIKI WATOKA NA MAAZIMIO 42 KUBORESHA SEKTA ZA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ameshiriki kwenye kikao cha kawaida cha mawaziri wa kilimo, mifugo na uvuvi katika ukanda wa Afrika Mashariki ambacho kimetoka na maazimio 42.

Akizungumza mara baada ya kutia sainia makubaliano hayo mawaziri wa nchi hizo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Afrika Mashariki (EACC) jijini Arusha Waziri Mpina ametaja maazimio manne kati ya 42 ambayo yanalenga kubiresha sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.

Waziri Mpina amesema azimio la kwanza ni nchi za Afrika Mashariki kuhakikisha zinazalisha chakula kwa kuongeza uzalishaji na kuweka mikakati itakayowezesha kuwa na uzalishaji wa kutosha na kujitosheleza kwa chakula.

Pili, kufanya biashara ya mazao ya chakula mifugo na uvuvi kwa nchi za Afrika Mashariki kuwa na takwimu za kujua kila nchi inafanya nini kwa kuwa na mfumo wa kupata takwimu kwa kutumia mfumo wa aina moja.

Tatu, vijana wanaoshughulika na kilimo, mifugo na uvuvi wengi wameshindwa kujiajiri na kuajiriwa nchi za Afrika Mashariki zimetoka na azimimo la kuandaa mikakati ya vijana kujiajiri na kuajiriwa katika sekta walizosomea za kilimo, mifugo na uvuvi.

Aidha Waziri Mpina ametaja azimimo lingine kuwa ni kutambua shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi ziende sambamba na usimamizi wa matumizi ya kemikali hivyo kuzitumia kwa umakini ili zisidhuru wananchi na mifugo.

Nchi zilizoshiriki kwenye kikao hicho ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akitoa tathmini mara baada ya kusainiwa kwa maazimio 42 kwa nchi za Afrika Mashariki yenye lengo la kuboresha sekta za kilimo, mifugo na uvuvi. (27.09.2019)

 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina pamoja na mawaziri wengine wa nchi za Afrika Mashariki wakitia saini maazimio 42 kwenye kikao cha kawaida cha mawaziri wa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, ambapo maazimio hayo yanalenga kuboresha sekta hizo. (27.09.2019)

 


Waliosimama Kutoka kulia: Makatibu wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah (Uvuvi) na Prof. Elisante Ole Gabriel (Mifugo) washuhudia utiaji saini wa maazimio 42 kwa mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kwenye ukumbi wa mikutano wa EACC jijini Arusha. (27.09.2019)Picha ya pamoja ya mawaziri katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi mara baada ya kusaini maazimio 42 kwa ajili ya kuboresha sekta hizo, kufuatia kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa EACC jijini Arusha. (27.09.2019)


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni