Nav bar

Jumatatu, 13 Novemba 2017

UZINDUZI WA NDEGE YA DORIA YA UVUVI KUTOKA MAURITIUS

Uzinduzi wa ndege ya doria inayoitwa Dornier 228 kutoka Serikali ya  Mauritius kwa ajili ya kupambana na  Uvuvi haramu.

Operesheni hii imeshirikisha nchi zote za Magharibi ya Bahari ya Hindi, ambapo ndege ya Coast Guard kutoka serikali  ya Mauritius inatumika kwa ajili ya kufanya doria ili kidhibiti uvuvi haramu.

Bw Hosea Mbilinyi DG Deep Sea Fishing Authority alisema kwenye operesheni za anga uvuvi tunalipa dola 32 na kuchangia asilimia 20 -40 katika kushirikiana kufanya doria ili kudhibiti eneo la uchumi wa bahari.

Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili  Mifugo na Uvuvi kutoka Zanzibar Hemed Rashid alisema tunatakiwa kulinda Rasilimali za uvuvi na kuwasaidia watanzania ili kuhakikisha nchi inabaki salama na lengo hasa ni Kujenga masoko ya kuunganisha sekta ya uvuvi na Utalii, ambapo mtalii anaweza kuingia na kununua bidha.

Aliendelea kusema Mhe. Waziri "ndani ya uvuvi haramu unaweza kukuta watu wanasafirisha vitu haramu, hvyo tunaomba wananchi wakaelewa bila kulinda rasilimali zetu sisi wenyewe tutaharibu mazao yetu".

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega alisema tujitahidi kutokomeza uvuvi haramu inaturudisha nyuma watanzania.
Operesheni inayofanyika ni kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu kwa kufanya doria kwenye anga na maji yetu  kwa kutumia meli na ndege ambapo inashikirikiana kufanya doria kenya na Tanzania.

Hivyo wanashirikiana maafisa kutoka Nchi zote za Magharibi ya Bahari ya Hindi zinazohusika zikiwemo Tanzania,  seychelles, Comoros, Mauritius, Reunion, Mozambique na kuwasiliana angani kama meli ya uvuvi imeonekana Kenya au Tanzania ikivua haramu.
Captain wa ndege hiyo Bw. Anshui Sharma akitoa maelezo mafupi kwa Mawaziri kuhusu ndege hiyo ya doria

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni