Nav bar

Jumatatu, 13 Novemba 2017

CHAMA CHA WANAWAKE (TAWLAE)

Chama cha wanawake  wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo,Uvuvi na Mazingira, Tanzania association of women leaders in agriculture and environment  ( TAWLAE) leo wamefungua rasimi mkutano wa mwaka  wa 21 na kuhudhuriwa na Naibu katibu Mkuu Bi Butamo Philipo kwa  niaba ya waziri wa  Mazingira  Mhe. January Makamba ambao umefanyika  leo katika viwanja vya wizara ya mifugo na uvuvi.

Akiongea katika mkutano huo wenyekiti ya chama cha wanawake viongozi katika kilimo na mazingira Dkt. Sofia Malote amesema Lengo kubwa la mkutano huo ni kuunganisha wakulima na tafiti mbalimbali  zilizoandaliwa na wataalamu hao

 "Maadhimisho ambayo yamebeba kaulimbiu isemayo  uchumi wa viwanda Tanzania wanawake tupo tayari,hapa ni kazi tu".


Aidha Dkt. Sofia Malote amesema kazi ya TAWLAE ni kuwaunganisha wakulima wadogo au wakubwa na tafiti mbalimbali ambaozo  zimetafitiwa hapa nchini  ili kuongeza uwekezaji na ajira kwa watanzania katika kilimo.Akizungumza  katika wasilisho lake Dkt.Malote amesema kilimo kilikuwa na faida ndogo kwa sababu utalaam,teknolojia na juhudi zilikuwa bado hazijatumika vizuri katika kilimo.


Ili kuingia katika uchumi wa viwanda  ni lazima uzalishaji  wa kilimo uwe na  tija uwepo na uboreshaji wa masoko na teknolojia ambapo wataalamu wanawake ndio wanajukumu kubwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo alisema Dkt.Malote

wanawake wakimkaribisha mgeni rasmi

Mgeni rasmi Bi. Butamo Philipo akitoa maelezo machache kwa wanawake wa TAWLAE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni