Nav bar

Jumamosi, 8 Agosti 2015

MHE. RAIS AFUNGA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANENAE 2015 KITAIFA MKOANI LINDI TAREHE 8/08/2015

 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho kikwete  akitoa hotuba ya kuhitimisha Maonesho ya sikukuu ya Wakulima 2015 Kitaifa yaliyofanyika Mkoani lindi katika Viwanja vya Ngongo.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akiendelea kutoa hotuba  ya kuhitimisha Maonesho ya Nanenane ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwaaga Wakulima na Wadau wa Kilimo kutokana na Sherehe za mwaka huu kuwa za mwisho katika kipindi chake cha Urais.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernad Membe akitaka tuimarishe ujirani mwema na Nchi Jirani kwa Maendeleo ya Wananchi wa Nchi zote

Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Mhe. Stephen M . Wasira Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika tayari kukabidhi  zawadi kwa Washindi wa maonesho hayo ya Wakulima na Wafugaji

 Wizara ya Maendeleo ya  Mifugo na Uvuvi imepata ushindi wa pili wa Wizara za Sekta ya Uchumi iliopokelewa na Mkurugenzi Bi. Anunciata Njombe Idara ya Uzalishaji Mifugo na Uendelezaji wa Masoko
Bw. Nicholai Chiweka Afisa Masoko na Utafiti apokea zawadi  ya kuwa Washindi wa pili katika Bodi ya Mazao kwa niaba ya Bodi ya Maziwa

Bw. Nicholai Chiweka Afisa Masoko na Utafiti wa  Bodi ya Nyama wakishangilia Ushindi pamoja na Bw. Mchome Heriel Meneja Utafiti na Ushauri  Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho kikwete azindua Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) (hayupo pichani)

Bendi ikitumbuiza kwenye Sherehe za Sikukuu ya Wakulima ya Nanenane katika Kiwanja cha Ngongo Mkoani Lindi
Kikombe cha Ushindi wa pili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni