Machapisho

MAABARA YA KISASA YA UTAFITI KATIKA SEKTA YA UVUVI NCHINI YAJENGWA KUPITIA MRADI WA SWIOFISH

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah amesema serikali imetilia mkazo suala la utafiti katika sekta ya uvuvi nchini ili kuhakikisha inapata taarifa sahihi ya maeneo ya mavuvi, kuzalisha vifaranga bora vya samaki pamoja na chakula bora cha samaki.   Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya kisasa ya utafiti wa uvuvi itakayotumika na Taasisi ya Utafiti Uvuvi Tanzania (TAFIRI) inayojengwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH), Dkt. Tamatamah amesema mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa mkopo wa masharti nafuu wa Shilingi Bilioni 2.6 unalenga kukuza sekta ya uvuvi nchini. “Kwenye uchumi wa bluu katika awamu hii tunategemea kununua meli nane kwenye uvuvi wa bahari kuu hivyo unapofanya uvuvi wa bahari kuu haujiendei tu lazima watafiti kama TAFIRI waende baharini wajue chambo wana...

DKT. TAMATAMAH ARIDHISHWA NA MATOKEO CHANYA YA MRADI WA SWIOFISH

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili katika mikoa ya Pwani na Tanga na kubainisha kuridhishwa na ujenzi wa majengo maalum kwa ajili ya ofisi za Vikundi vya Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi (BMU) kupitia Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH).   Akizungumza na viongozi wa BMU na wananchi kwa nyakati tofauti mara baada ya kutembelea majengo hayo kwenye kata ya Dunda, wilaya ya Bagamoyo na kata ya Saadani, wilaya ya Chalinze katika mkoa wa Pwani, kata ya Kipumbwi, wilaya ya Pangani na kata ya Zingibari, wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Dkt. Tamatamah amesema ujenzi wa majengo hayo unaendelea vizuri huku akiwataka makandarasi kuhakikisha majengo hayo yanakamilika ifikapo mwezi Desemba Mwaka 2020 kama makubaliano yalivyo kwenye mikataba.   “Nimeridhishwa na ujenzi wa baadhi ya majengo hayo kupitia mradi wa SWIO...

WIZARA YAFANYA UKAGUZI WA UKARABATI WA BWAWA LA MAJI KWA AJILI YA MATUMIZI YA MIFUGO NA BINADAMU

Picha
  Mhandisi kutoka Kampuni ya ZECO, Emmanuel Rodrick (kushoto) akitoa maelezo kwa Mhandisi kutoka WMUV, Masanga Makoje (mwenye flana ya njano) jinsi maji yaliyotokana na mvua kubwa, yalivyobomoa ukingo uliokarabatiwa na hatua zitakazochukuliwa kurekebisha hali hiyo ili maji yajae. Bwawa hilo lipo katika kijiji cha Narakauo, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara. (16.11.2020) Mhandisi Masanga Makoje (kulia) akiwa na Mhandisi wa Kampuni ya ZECO, Emmanuel Rodrick wakikagua ukarabati wa bwawa la maji kwa ajili ya matumizi ya Mifugo na Binadamu katika kijiji cha Narakauo, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara. (16.11.2020) Mhandisi kutoka WMUV, Masanga Makoje (mwenye flana ya njano kushoto) akitoa maelezo ya ushauri kwa Mhandisi wa Kampuni ya ZECO, Emmanuel Rodrick kuhusu ukarabati wa bwawa la maji kwa ajili ya matumizi ya Mifugo na Binadamu unaoendelea kufanyika katika bwawa hilo kwenye kijiji cha Narakauo, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara. (16.11.2020) Bwawa la maji kwa ajili ya matumizi y...

SERIKALI KUIMARISHA UVUVI WA BAHARI KUU

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  John Pombe Joseph Magufuli amesema kuwa katika kipindi cha miaka 5 ijayo ya awamu yake ya pili ya uongozi atahakikisha sekta ya uvuvi inakuzwa ikiwemo kuimarisha shughuli za uvuvi wa bahari kuu kwa kununua Meli nane (8) zitakazofanya kazi katika ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi ulioko Visiwani Zanzibar na Tanzania bara. Dkt. Magufuli aliyasema hayo wakati akitoa hotuba yake ya kulifungua Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma Novemba 13, 2020. Wakati akilihutubia bunge hilo lililosheheni Wabunge wengi wapya, Dkt. Magufuli alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo mengi yanayofaa kwa shughuli za uvuvi ikiwemo Mito, Bahari na Maziwa hali ambayo inaifanya sekta ya uvuvi kuwa na nafasi kubwa ya kutoa mchango katika kukuza pato la taifa, kupambana na umasikini na tatizo la ajira. Alisema pamoja na fursa hiyo iliyopo nchini bado mpaka sasa mchango wa sekta ya uvuvi upo chini hivyo serikali imekusudia kuwekeza nguvu ...

NI MARUFUKU KULISHA MIFUGO VYAKULA VIBOVU - SERIKALI.

Picha
Serikali imepiga marufuku matumizi ya vyakula vilivyopoteza ubora wa kutumiwa na binadamu na kutumiwa kama vyakula vya mifugo kabla ya kuthibitishwa kwanza na wataalam wa maabara ya mifugo.   Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo (WMUV), Dkt. Asimwe Rwiguza ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya siku mbili ya wakaguzi wa vyakula vya mifugo kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Singida na yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.   "Kumekuwa na mazoea ya vyakula ambavyo vimeshapoteza ubora wa matumizi ya binadamu kutumika kama vyakula vya mifugo hivyo ninapenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa wafugaji, wazalishaji na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na uzalishaji wa vyakula vya binadamu kuwa ni marufuku kutumia vyakula hivyo bila Wizara yenye dhamana kuwa na taarifa na kujiridhisha kitaalam kama chakula hicho kinafaa au la," Amesisitiza Dkt. Rwiguza.   Aidha, Dkt. ...

WAFUGAJI WAKIJENGEWA UWEZO WATAKUZA UCHUMI WA TAIFA - MONGELA.

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela amesifu juhudi zinazofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuhakikisha wafugaji wake wanafanya shughuli hiyo kwa tija na kwa kuzingatia dhana ya ukuzaji wa uchumi wao.   Mhe. Mongela ameyasema hayo leo (12.11.2020) baada ya kupokea timu ya wataalam wa Idara ya Uendelezaji Malisho na Rasilimali za vyakula vya mifugo (Wizara ya Mifugo na Uvuvi) ambao wamefika mkoani humo kwa ajili ya kutoa mafunzo ya siku mbili kwa wakaguzi wa vyakula vya mifugo kuhusu ukaguzi wa maeneo ya malisho na rasilimali za vyakula vya Mifugo   "Tunajitahidi sana kukuza tasnia ya ufugaji lakini uwepo mafunzo kama haya unawafanya wafugaji wetu wasiishie tu kufuga bali wafuge kwa tija na kukuza uchumi wao" amesema Mhe. Mongela.   Mhe. Mongela ameishauri Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuendelea na jitihada hizo za kujenga uwezo kwa wafugaji ili kuwafanya kuwa wafugaji bora wenye uelewa na ujuzi wa ufugaji wa kisasa badala ya ufugaji wa asili ambao hau...

SERIKALI YATUMIA SH. MILIONI 900 KUKARABATI MABWAWA MAWILI YA KUNYWESHEA MIFUGO

Picha
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa serikali inatumia zaidi ya shilingi Milioni 900 kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa wa Mabwawa mawili ya kunyweshea mifugo ya Narakauo lililopo Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara na Bwawa la Kimokuwa lililopo Wilayani Longido, Mkoani Arusha.   Prof. Gabriel alieleza hayo alipokuwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa mabwawa hayo katika Mikoa ya Arusha na Manyara Novemba 7, 2020.   Akiongea na Wafugaji wa maeneo hayo baada ya kufanya ziara hiyo, Prof. Gabriel alisema kuwa bwawa la Narakauo limetengewa milioni 413 wakati bwawa la Kimokuwa limetengewa milioni 511.9.   Prof. Gabriel alieleza kuwa ukarabati huo ni utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli alipokuwa Mkoani Manyara hivi karibuni ya kuhakikisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi inafanya jitihada za dhati kutatua changamoto ya maji kwa mifugo.   Aliongeza kuwa, mb...