Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng'wasi Kamani amewataka wajasiriamali 350 wa sekta ya uvuvi waliopata mafunzo ya kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi kutumia ujuzi walioupata kwa ajili ya kuongeza ajira, Kipato na kuchagia Maendeleo ya Taifa.
Akizungumza wakati wa kufunga
Mafunzo hayo Leo Januari 9, 2026 katika Ukumbi wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya
Uvuvi (FETA) Kampasi ya Nyegezi Mhe. Kamani amesema serikali inaendelea kuunga
Mkono wajasiriamali wanaojihusisha na uongezaji wa thamani ya mazao ya uvuvi
ili kupanua biashara zao.
"Mafunzo hayo yanaakisi
dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya
kuwawezesha wananchi kiuchumi, hususan wanawake na vijana, kupitia fursa za
Uchumi wa Buluu, leo mnapopewa vyeti mnakabidhiwa dhima ya kwenda kutumia ujuzi
wenu kuongeza ajira, kipato na maendeleo ya Taifa” alisema Mhe. Kamani.
Aidha, aliongeza kuwa serikali
imetenga kiasi cha shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa
miundombinu ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi ili kuongeza ufanisi
unaolenga kutoa mafunzo bora ya kukuza sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu
Kwa Upande wake, Mtendaji Mkuu wa
Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Dkt. Semvua Mzighani amesema mafunzo
hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ubelgiji la ENABEL kupitia
mradi wa Green and Smart Cities (IncluCities) yamelenga kuongeza thamani ya
mazao ya uvuvi, ushindani wa bidhaa sokoni na kuongeza kipato cha kaya.
Awali wawakilishi wa Kundi la Vijana na Kina
Mama Wajasiriliamali wakiwasilisha risala yao kwa mgeni rasmi walieleza kuwa
mafunzo hayo yataenda kubadilisha mfumo mzima wa uchakataji na uongezaji wa
thamani wa mazao ya Uvuvi tofauti na hapo awali walipokuwa wakitumia njia za
jadi.
Jumla ya kina mama wajasiriamali
200 wamehitimu mafunzo ya usindikaji wa mazao ya samaki, huku vijana 150
wakipata mafunzo ya utayari kazini katika ukuzaji viumbe maji.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni