Nav bar

Jumatano, 1 Oktoba 2025

TVLA YATOA JEZI KWA TIMU YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

◼️Zatambulishwa rasmi tayari kuanza kutumika

Maabara ya Veterinari nchini (TVLA) imeendelea na utaratibu wake wa kuunga mkono tasnia ya michezo nchini hususan upande wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi baada ya kuikabidhi  timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi jezi na vifaa mbalimbali vya michezo inayoshiriki kwenye michuano ya SHIMIWI inayoendelea hivi sasa jijini Mwanza.

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Mwenyekiti wa SHIMIWI Wizarani hapo Bw. Sebastian Shilangalila amemshukuru Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt. Stella Bitanyi kwa msaada huo ambao ameweka wazi umeongeza morali kwa wachezaji wa timu zote zinazoshiriki michuano hiyo.

“TVLA wamekuwa wakituunga mkono kwenye michuano hii kila mwaka, hivyo nitoe shukran za dhati kwao kwa niaba ya viongozi wenzangu na wachezaji wa michezo yote tunayoshiriki na nitoe rai kwa wadau wengine kujitokeza kuunga mkono jitihada hizo” Ameongeza Bw. Shilangalila.

Vifaa vya michezo vilivyotolewa na Wakala hiyo ni pamoja na Jozi mbili za jezi za mpira wa miguu, jozi moja ya mpira wa pete, jozi moja ya timu ya kuvuta kamba (wanawake), mipira miwili ya mchezo wa mpira wa Miguu na mmoja wa Pete.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni