◼️Wafuzu fainali riadha mita 100
◼️Washika nafasi ya 2 Tufe (Wanawake) na nafasi ya 3 (Wanaume)
Timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kupeperusha vema bendera yao kwenye michuano ya SHIMIWI iliyoendelea leo Septemba 08,2025 jijini Mwanza baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo 3 tofauti ikianza na mchezo wa kamba hatua ya 16 bora iliyoikutanisha na timu ya Wizara ya Elimu na kufanikiwa kuwavuta kwa mivuto yote miwili.
Mara baada ya mchezo huo, Wachezaji wa mchezo wa riadha kutoka Wizarani hapo wakaingia dimbani kufukuza upepo ambapo mchezaji Valentino Kikoti amefanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya mbio za umbali wa mita 100 huku upande wa mchezi wa kurusha tufe (Wanawake) ukiwakilishwa vema na Theodata Salema aliyeshika nafasi ya pili na upande wa wanaume ukiwa salama kupitia kwa mchezaji Alfred Mushi aliyefanikiwa kushika nafasi ya 3 baada ya kurusha tufe umbali wa mita 8.90 kwenye mchezo uliokuwa na upinzani mkali.
Kufutia matokeo hayo vikosi vya Wizara ya Mifugo na Uvuvi vinaelekeza nguvu zake katika hatua inayofuata ambapo Kamba (Wanaume) wanasubiri kufahamu mpinzani wao kwenye hatua ya robo fainali huku fainali ya mchezo wa Riadha ikitarajiwa kufanyika Septemba 10,2025.
Aidha Wizara hiyo itashiriki katika mbio za umbali wa mita 1500 na michezo ya jadi inayotarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia kesho (Septemba 09,2025) kwenye Viwanja vya CCM Kirumba.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni