Nav bar

Jumatano, 1 Oktoba 2025

KAMBA WANAUME WATINGA ROBO FAINALI KWA JASHO NA DAMU

◼️Waivuta Wizara ya Ardhi “Mvuto wa Dhahabu” baada ya kutoshana nguvu kwenye michezo miwili ya awali.

Timu ya mchezo wa kuvuta kamba kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya SHIMIWI inayoendelea jijini mwanza kibabe kwa kuongoza kundi lao baada ya kuivuta timu ya Wizara ya Ardhi kwa “mvuto wa dhahabu” kwenye mchezo uliokuwa na upinzani mkali kutoka pande zote mbili uliochezwa leo Septemba 05,2025.

Matokeo hayo yametokana na raundi ya kwanza ya mchezo huo ulioteka macho ya mashabiki wote kwenye uwanja wa Furahisha kukamilika kwa kila timu kushinda mvuto mmoja hatua iliyoilazimu kamati ya mashindano hayo kurusha shilingi iliyoamua kipindi kimoja cha marudio ya mchezo huo (Mvuto wa Dhahabu).

Mchezo wa leo unafuatia matokeo ya mchezo wa awali baina ya timu hizo uliochezwa Septemba 03,2025  ambapo timu zote zilitoshana nguvu huku zikiwa zimelingana alama na hivyo kuilazimu kamati ya mashindano kuamuru mchezo huo urudiwe ili ipatikane timu itakayoongoza kundi.

Aidha matokeo ya leo yanaifanya timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufuzu hatua ya robo fainali ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja kwenye michuano hiyo.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni