Nav bar

Jumatano, 6 Agosti 2025

MAJALIWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO SEKTA YA UFUGAJI SAMAKI

Na. Omary Mtamike

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameridhishwa na maendeleo ya Sekta ya Ufugaji wa samaki nchini ambapo amewataka wananchi kuelekeza nguvu kwenye tasnia hiyo ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa samaki nchini.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo Agosti 03, 2025 mara baada ya kufika kwenye eneo la mabwawa ya ufugaji samaki na vizimba lililopo kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya kimataifa ya Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

“Mhe. Rais amesambaza vizimba vingi vya kutosha kanda ya ziwa, nilitaka kufahamu kama tumefanikiwa” amesema Mhe. Majaliwa.

Aidha Mhe. Majaliwa ameridhishwa na gharama ya vizimba hivyo ambayo amekiri hata watu wa kipato cha chini wanaweza kuimudu huku pia akitoa rai kwa wananchi wote hususani wadau wa Uvuvi kutumia zana zilizoidhinishwa na Serikali wakati wote wa utekelezaji wa shughuli zao za Uvuvi.

Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzake wa mkopo wa masharti nafuu wa vizimba hivyo Makamu mwenyekiti kutoka kikundi cha Vijana Kazini kutoka mkoani Mwanza Bw. Elisha Gayo ameishukuru Serikali kwa mkopo wa shilingi milioni 117 waliopatiwa ambapo amekiri umesaidia kubadili maisha yao kwa kiasi kikubwa.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa Maelekezo kwa Viongozi na Watendaji  wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  alipotembelea na kukagua Mabwawa ya Kufugia Samaki kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane Nzuguni Jijini Dodoma Agosti 3, 2025.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena (Watatu, kushoto) akimwelezea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa yanayopatikana kwa upande wa Sekta ya ukuzaji Viumbe Maji kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane Nzuguni Jijini Dodoma Agosti 3, 2025.

Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Madala (Wa Kwanza Kulia) akifafanua mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa aina za vizimba vya kufugia samaki vilivyopo kwenye eneo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Waziri kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane Nzuguni Jijini Dodoma Agosti 3, 2025.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni