Nav bar

Alhamisi, 15 Mei 2025

SERIKALI IMEWATAKA WAVUVI KUSALIMISHA ZANA HARAMU ZA UVUVI

 Na. Stanley Brayton, WMUV

Kipili, Nkasi, Rukwa

Mei 14, 2025

Serikali, kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), imewataka wavuvi wote nchini, ambao si waaminifu, kusalimisha zana zao za uvuvi haramu kwa hiari yao wenyewe badala ya kusubiri kufuatwa huko walikojificha na kufanya vitendo vya uvuvi haramu.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede wakati akizungumza na baadhi ya wavuvi na wadau wa uvuvi wa Ziwa Tanganyika katika ziara yake ya kufuatilia shughuli za doria zinavyofanyika na kujua maendeleo na changamoto wanazokutana nazo watumishi wa Serikali katika kufanya doria kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika, leo Mei 14, 2025, katika Kijiji cha Kipili, Wilayani Nkasi, Mkoani Rukwa.

“Ninyi wenyewe wananchi na wavuvi mmesema kwa vinywa vyenu kuwa kuna wavuvi bado wameficha zana haramu za uvuvi majumbani na sehemu mbalimbali, sasa ninawaambia kuwa hizo zana haramu za uvuvi mzisalimishe katika Mamlaka husika ili tuondokane na adha zitokanazo na uvuvi haramu na pia tuwe na uhakika wa uendelevu wa Ziwa letu," amesema Dkt. Mhede.

Vilevile, Dkt. Mhede amewataka wavuvi kuwaambia wavuvi wenzao kuwa wasisubiri kufuatwa na Mamlaka husika maana watafuatwa katika msako unaoendelea na hatimae Sheria itafuata mkondo wake dhidi ya watakaobainika.

Aidha, Dkt. Mhede amewataka na kuwasihi wavuvi wa Ziwa Tanganyika kutofanya uvuvi haramu sio kwa vitendo tu bali pia kwa kufichiana siri, na watoe taarifa kwenye Mamlaka husika ili hatua zichukuliwe kwa baadhi ya wavuvi au mawakala wa wavuvi wasio waaminifu.

Halikadhalika, Dkt. Mhede amewataka Maafisa Uvuvi kutenda kazi zao kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa kisheria ambapo ameelekeza kuwa kutoza ushuru wa mazao ya uvuvi yaliyovunwa kwa njia haramu (mfano samaki wachanga) nalo ni kosa. Amesisitiza kwamba Serikali inatilia mkazo katika kutoza maduhuli kwa mazao ya uvuvi yaliyovunwa kihalali na sio yaliyovunwa kwa njia haramu.

Naye, Mvuvi wa Ziwa Tanganyika, Bw. Juma Yahya, aliongea kwa niaba ya wavuvi wenzake, na kuishukuru Serikali ya awamu ya Sita ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa hatua walizozichukua katika kudhibiti na kuhakikisha zana za Uvuvi haramu katika Ziwa Tanganyika zinatokomezwa.

Bw. Yahya, ameiomba Serikali kupitia Wizai ya Mifugo na Uvuvi kuongeza Doria ili kuweka Usalama wa mazao ya Uvuvi na wavuvi wenyewe.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede (wa kwanza kulia), akikagua nyavu haramu zilizokamatwa kutoka kwa Wavuvi, wakati wa ziara yake ya kufuatilia shughuli  za Doria zinavyofanyika na kujua Maendeleo na Changamoto wanazokutana nazo Maafisa katika kufanya Doria katika Ziwa Tanganyika, Mei 14, 2025 Nkasi - Rukwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede akizungumza na wavuvi wa Ziwa Tanganyika, wakati wa ziara yake ya kufuatilia shughuli  za Doria zinavyofanyika na kujua Maendeleo na Changamoto wanazokutana nazo Maafisa katika kufanya Doria katika Ziwa Tanganyika, Mei 14, 2025 Nkasi - Rukwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni, wakati wa ziara yake ya kufuatilia shughuli  za Doria zinavyofanyika na kujua Maendeleo na Changamoto wanazokutana nazo Maafisa katika kufanya Doria katika Ziwa Tanganyika, Mei 14, 2025 Nkasi - Rukwa.

Mkurugenzi wa Uvuvi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh, akitoa neno la utangulizi kabla ya ukaguzi wa shughuli za Doria katika Kituo cha Kipili, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) ya kufuatilia shughuli  za Doria zinavyofanyika na kujua Maendeleo na Changamoto wanazokutana nazo Watumishi katika Doria, Mei 14, 2025 Nkasi - Rukwa.

Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Kitengo cha Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Kimasa Bugomba, akielezea hali ya awali kuhusiana na Utekelezaji wa zoezi maalumu la Doria katika kudhibiti Uvuvi haramu Ziwa Tanganyika, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara  ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) ya kufuatilia shughuli  za Doria zinavyofanyika na kujua Maendeleo na Changamoto wanazokutana nazo Watumishi katika Doria, Mei 14, 2025 Nkasi - Rukwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede (wa tatu kulia), akipokea  pongezi kutoka kwa Wavuvi wa Ziwa Tanganyika katika kutokomeza Uvuvi haramu na kusikiliza maombi yao kwa Serikali na Changamoto zinazowakumba katika shughuli zao za Uvuvi, wakati wa ziara yake ya kufuatilia shughuli  za Doria zinavyofanyika na kujua Maendeleo na Changamoto wanazokutana nazo Maafisa katika kufanya Doria katika Ziwa Tanganyika, Mei 14, 2025 Nkasi - Rukwa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni