Nav bar

Alhamisi, 15 Mei 2025

NIGERIA YAVUTIWA NA MPANGO KABAMBE WA MIFUGO TANZANIA

Na Chiku Makwai- WMUV

Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo ya nchini Nigeria ikiongozwa na Mkurugenzi Mratibu wa Programu za Kitaifa wa Wizara hiyo,  Dkt. Ishiyaku Mohammed imeonesha kuvutiwa na namna Tanzania inavyotekeleza Mpango Kabambe wa Mifugo Tanzania (Tanzania Livestock Master Plan) katika kuboresha sekta ya mifugo.

Hayo yamefahamika wakati wa kikao baina ya Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe na timu hiyo ya Wataalamu kutoka nchini na Nigeria kilichofanyika katika ofisi za wizara zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma leo Mei 13, 2025.

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Mohammed amesema kuwa lengo la ziara yao ni kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna Tanzania ilivyofanikiwa kutekeleza mpango kabambe huo ili iwasaidia katika kufanya maandalizi ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Mifugo wa Nigeria (NLMP) wanaotarajia kuuanzisha.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe ameieleza timu hiyo kuwa Serikali imeendelea kuimarisha sekta ya mifugo kupitia Mpango Kabambe huo ambao umechangia kuboresha maeneo ya Afya ya Mifugo, Malisho na Maji pamoja na kuzalisha Mbegu Bora.

Aidha, Prof. Shemdoe ameongeza kuwa pamoja na mpango huo serikali imeandaa kampeni ya chanjo kwa mifugo inayotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itakayo saidia mifugo kuwa na afya bora ili kukidhi vigezo vya soko la kimataifa.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wageni kutoka Nigeria waliokuja kujifunza jinsi Mpango Kabambe wa Mifugo Tanzani ulivyotekelezwa nchini humo kilichofanyika Mei 13, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo mji wa Serikali Mtumba


Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Stephen Michael akiwasilisha programu ya Mpango Kabambe wa Mifugo Tanzania wakati wa kikao cha Wageni kutoka Nigeria waliokuja kujifunza jinsi Mpango huo ulivyotekelezwa nchini Tanzania kilichofanyika Mei 13, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo mji wa Serikali Mtumba.

Kiongozi wa Msafara ambaye ni Mkurugenzi Mratibu wa Programu za Kitaifa Dr.  Ishiyaku Mohammed akiwasilisha Mpango Kabambe wa Mifugo Nigeria (NLMP) ulioandaliwa nchini Kwao kwa Lengo la kupata maini kwajili ya utekelezaji wa mpango huo wakati wa kikao hicho kilichofanyika Mei 13, 2025 mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa tano kutoka kulia)  akiwa kwenye Picha ya pamoja wageni kutoka Nchini Nigeria walioambatana na uongozi wa taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (IRLI) pamoja na baadhi ya watendaji wake baada ya kikao na wageni hao kilichofanyika Mei 14, 2025 jiijini  Dodoma.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni