Nav bar

Jumatano, 29 Septemba 2021

KIKAO NA WAFAWIDHI WANAOZALISHA VIFARANGA VYA SAMAKI NA KUKUSANYA MADUHULI JIJINI DODOMA.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akiongea na wafawidhi wanaozalisha vifaranga vya samaki na kukusanya maduhuli (hawapo pichani). Aidha amewapongeza kwa kazi wanayofanya na kuwataka kufanya kazi kibiashara na matokeo yaonekane na sio kufanya kazi kwa mazoea. Kikao hicho kilifanyika  Jijini Dodoma Septemba16, 2021.

Mtaalam wa Programu za Kielekroniki, Clemence Mutalemwa akimuonesha Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) demo ya namna mfumo tumizi utakavyorahisisha huduma za ugani na taarifa za Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya simu ya kiganjani katika kikao kilichofanyika Jijini Dodoma Septemba 16, 2021. Aliyesimama ni Mkurugenzi, Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt Nazael Madalla.

 


 Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafawidhi wanaozalisha vifaranga vya samaki na kukusanya maduhuli kwenye vituo mbalimbali vya Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Kushoto ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madalla na kulia ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Baridi, Dkt. Imani Kapinga muda mfupi baada ya kumaliza kikao  kilichofanyika Jijini Dodoma Septemba 16, 2021.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni