Nav bar

Alhamisi, 5 Agosti 2021

KATIBU MKUU, WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI, (MIFUGO) PROF. ELISANTE OLE GABRIEL VISIWANI ZANZIBAR.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea na  Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo (Zanzibar), Dkt. Soud Hassan alipomtembelea Waziri huyo Ofisini kwake. Prof. Ole Gabriel alifanya ziara  Visiwani Zanzibar Agosti 2, 2021 kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano baina ya Sekta ya Mifugo, Tanzania bara na Sekta ya Mifugo,  Zanzibar, pia kufanya uhamasishaji wa ufugaji wa kisasa Visiwani humo. 

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akikagua moja kati ya aina mbalimbali za malisho ya mifugo zinazofanyiwa Utafiti  na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo, Zanzibar (ZALIRI) alipotembelea taasisi hiyo iliyopo Visiwani Zanzibar Agosti 2, 2021. 

 

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kushoto) akiongea na Viongozi wa Kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Azam Kilichopo Fumba, Visiwani Zanzibar. Prof. Ole Gabriel alifanya ziara katika Kiwanda  hicho Agosti 2, 2021 kwa lengo la  kukagua maendeleo yake ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kuendelee kuzalisha maziwa kwa kiwango kilichokusudiwa  huku akiwaeleza kuwa Serikali ipo pamoja nao. Katikati ni Meneja wa Kiwanda hicho, Adilson Fagundes na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Udhibiti Ubora wa bidhaa katika Kiwanda hicho, Tumaini Fredrick. 

 


 

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Zanzibar, Dkt. Soud Hassan (katikati). Prof. Ole Gabriel alimtembelea Waziri huyo Ofisini kwake, Visiwani Zanzibar Agosti 2, 2021. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni