Nav bar

Alhamisi, 18 Februari 2021

PROF. GABRIEL AELEZA KWA UFUPI UMUHIMU WA KIWANDA CHA ACE LEATHER TANZANIA Ltd.

 

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akieleza kwa ufupi umuhimu wa Kiwanda cha Ace Leather Tanzania Ltd katika kuleta maendeleo ya Sekta ya Mifugo hususan katika tasnia ya ngozi mapema leo wakati wa uzinduzi wa Kiwanda hicho uliofanyika Mkoani Morogoro Februari 12, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kiwanda cha kuchakata Ngozi cha Ace Leather Tanzania Ltd kilichopo Kihonda, Mkoani Morogoro Februari 12, 2021. Kulia kwake ni Mmiliki wa Kiwanda hicho, Rostam Aziz. Wa kwanza kulia, mstari wa nyuma ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel. Wengine ni Viongozi Wakuu wa Serikali na baadhi ya wamiliki wa kiwanda hicho.


Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (katikati) walipokutana katika uzinduzi wa Kiwanda cha kuchakata Ngozi cha Ace Leather Tanzania Ltd uliofanyika Mkoani Morogoro leo Februari 12, 2021. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Morogoro Mjini, Georgina Matagi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni