Nav bar

Alhamisi, 18 Februari 2021

NARCO YATANGAZA TOZO MOJA KWA WAWEKEZAJI WAPYA WANAOKODISHA VITALU KATIKA RANCHI ZA TAIFA

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Kampuni ya Ranchi za Taifa, Bw. Paul Kimiti (katikati) akiongea na wadau wa sekta ya Mifugo kupitia vyombo vya habari kuhusu suala la tozo kuwa moja kwa wawekezaji wa wapya wanaokodisha vitalu vya Ranchi za Taifa na kwamba bei itakuwa ni shilingi 3,500 kwa ekari moja. Mkutano huo na waandishi wa habari umefanyika katika ukumbi wa Kitengo cha Baraza la Veterinari Tanzania, Jijini Dar es Salaam. (08.02.2021)


Meneja Masoko wa Kampuni ya Ranchi za Taifa, Bw. Emmanuel Mzava akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni za Ranchi za Taifa na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Kitengo cha Baraza la Veterinari Tanzania Jijini Dar es Salaam. (08.02.2021)


Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki kwenye mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Kitengo cha Baraza la Veterinari Tanzania Jijini Dar es Salaam. (08.02.2021)Hakuna maoni:

Chapisha Maoni