Nav bar

Jumanne, 15 Septemba 2020

TIMU YA WATAALAM MRADI WA SWIOfish YAFANYA UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA MRADI HUO DAR ES SALAAM, TANGA NA PWANI

Pichani ni Jengo jipya la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) linalojengwa Kunduchi, jijini Dar es Salaam kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mradi wa SWIOfish. Timu ya Wataalam kutoka SWIOfish ilitembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya ujenzi huo ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibuni. (11.09.2020)

Mratibu wa Mradi wa SWIOfish, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga, Asha Churu akieleza jambo kwa Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Zingibari na Viongozi wa BMU muda mfupi baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi unaondelea wa Ofisi ya BMU kijijini hapo. Timu ya Wataalam kutoka Mradi wa SWIOfish walitembelea Wilaya hiyo kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo. (12.09.2020)

Mwenyekiti wa Kijiji cha Zingibali, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga, Ibrahim Mahasham akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Ofisi ya BMU ya kijiji cha Zingibari kwa Timu ya Wataalam kutoka Mradi wa SWIOfish waliokwenda kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa mradi Wilayani humo. Ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa SWIOfish. (12.09.2020)

Timu ya Wataalam kutoka Mradi wa SWIOfish wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Zingibari na Viongozi wa BMU, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga walipotembelea kijiji hicho kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa SWIOfish. Katikati ni Afisa Mawasiliano, Mradi wa SWIOfish, Amina Kiaratu. Wa tatu kutoka kushoto ni Afisa Ufuatiliaji na Utathimini, Mradi wa SWIOfish, Furaha Kabuje na wa kwanza kulia ni Mratibu wa Mradi wa SWIOfish, Wilayani Mkinga, Asha Churu. (12.09.2020)

Mwenyekiti wa Kamati ya Takwimu ya BMU, Kijiji cha Kaole, Wilayani Bagamoyo, Salum Iddy (Kulia) akifafanua jambo kwa Timu ya Wataalam kutoka Mradi wa SWIOfish waliotembelea Wilaya ya Bagamoyo kufanya ufuatiliaji wa mafanikio ya utekelezaji wa Mradi wa SWIOfish. Wa pili kulia ni Afisa Ufuatiliaji na Utathimini kutoka Mradi wa SWIOfish, Furaha Kabuje. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Mradi wa SWIOfish, Amina Kiaratu. Wengine ni Viongozi wa BMU ya Kaole, Wilayani Bagamoyo. (11.09.2020)

Ujenzi wa Ofisi ya BMU ya Kijiji cha Zingibari, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga ukiwa katika hatua ya msingi kama inavyoonekana katika picha.






 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni