Nav bar

Ijumaa, 24 Julai 2020

MAKATIBU WAKUU WAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI YA NANE NANE 2020


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya leo (24.07.2020) ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kujadili maandalizi ya Maonesho ya Kilimo Nane nane yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu kuanzia tarehe 01 Agosti, 2020.

Katika kikao hicho, Bw. Kusaya  alieleza kuwa ni matarajio ya wizara ya kilimo na zile za kisekta kuona maonesho ya Nane nane mwaka huu yanakuwa tofauti katika kuleta mapinduzi ya, ufugaji na uvuvi ili wananchi wapate kuongeza tija na ufanisi kukuza uchumi wa kaya na taifa.

Kikao hicho kimehusisha Makatibu Wakuu ambao ni Prof. Riziki Shemdoe (Viwanda na Biashara), Prof. Elisante Ole Gabriel (Mifugo), Mhandisi Anthony Sanga (Maji) na Dkt. Rashid Tamatamah (Uvuvi) na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Miriam Mmbaga pamoja na kamati ya maandalizi.

“Tunapenda kuona maonesho ya Nane nane mwaka huu yanakuwa tofauti na yaliyopita katika kuwafanya wakulima, wafugaji na wavuvi  wabadilike kutoka katika  kilimo cha kujikimu kuwa kilimo, ufaguji na uvuvi wa kibiashara kupitia  elimu na teknolojia bora watakayojifunza kutoka kwa wataalam “ alisema Kusaya.

Kikao kimezishauri Wizara, taasisi na wadau wa maonesho ya mwaka huu kujikita katika kuwasaidia wakulima,wavuvi na wafugaji kuongeza tija katika shuguli zao ili baada ya maonesho maisha yao yawe bora zaidi kiuchumi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel alisema wakulima wanahitaji elimu ya kubadilisha mtizamo hivyo matumizi ya vyombo vya habari kufikisha elimu kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ni muhimu sana kwenye maonesho haya.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe alisema ni vema kamati ya uratibu ikaweka utaratibu wa kuwakutanisha wafanyabiashara za mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na wakulima kwenye maonesho hayo hususan Simiyu.

“Tuandae maeneo kwa ajili wa wafanyabiashara na wakulima, wafugaji na wavuvi kufanyia mazungumzo ya kukuza upatikanaji wa masoko na kutumia fursa za biashara ikiwemo kuwekeza katika viwanda” alisisitiza Prof. Shemdoe.

Maonesho ya Kilimo Nane nane mwaka huu yana kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020”.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ol Gabriel akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo.  (24.07.2020)

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo.  ( 24.07.2020)

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. (24.07.2020)

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo.  (24.07.2020)

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. (24.07.2020)

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bibi Miriam Mmbaga akizungumza kwenye kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo  (24.07.2020)

Sehemu ya wajumbe wakifuatilia kikao cha Makatibu Wakuu wa wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. ( 24.07.2020)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni