MATANGAZO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

          WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI


 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi imepanga kuajiri maafisa walioorodheshwa hapa chini katika mwaka 2011/12 hivyo tunapenda  kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa zilizoainishwa watume barua za maombi ya kazi zifuatazo:

2. Daktari Mifugo Mkufunzi Daraja la II (Veterinary Tutor II) (Nafasi 5)

(a)               Sifa za waombaji

Wawe wamehitimu Shahada ya kwanza  ya Sayansi ya tiba ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali waliosajiliwa na Bodi ya Madaktari wa Mifugo Tanzania

(b)               Majukumu

-                     Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo
-                     Kuandaa mtiririko  wa kila somo (lesson plan) kwa  upande wa nadharia na vitendo.
-                     Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada kwa  upande wa nadharia na vitendo.

·        Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.

·        Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.

·        Kufanya kazi nyingine zote kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

(c)                Mshahara

Mishahara ya watumishi wa Serikali ngazi ya TGS F.

3.Afisa Mifugo daraja la II (Livestock officer II) (Nafasi 128)

Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (kwenye Mashamba ya Uzalishaji Mifugo), Sekretarieti za  Mikoa, na Mamlaka za Mitaa.

(d)               Sifa za waombaji

Waombaji wawe wamehitimu Shahada ya Sayansi ya Mifugo (Animal Science) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokone au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

(e)                Majukumu
·        Atabuni mipango ya uzalishaji Mifugo Wilayani
·        Ataratibu uzalishaji wa Mifugo katika mashamba makubwa ya Mifugo
·        Atasaidia  kuratibu mipango ya Ugani kuhusiana na Uzalishaji wa Mifugo Wilayani.
·        Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataalam wa mifugo na wafugaji.
·        Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya Masoko ya Mifugo Wilayani kwake na Mkoani.
·        Atabuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo Wilayani.
·        Atafanya  Soroveya  ya rasilimali (resource survey) kwa mfano: mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.
·        Ataendesha mafunzo kwa wakala, na wataalamu juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
·        Atatafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali.
·        Atafanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
·        Atashiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibibu  wa malisho.
·        Ataandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
·        Atafuatilia,  kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
·        Atafanya kazi nyingine zinazohusiana  na fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

(f)                 Mshahara 
Mishahara ya watumishi wa Serikali ngazi ya TGS D.

4.Daktari wa Mifugo daraja II (Veterinary Officer II) (Nafasi 47)

Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi  Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (kwenye vituo vya Uchunguzi wa Afya za Mifugo), Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

(a)               Sifa za waombaji
Wawe wamehitimu shahada ya kwanza ya tiba ya mifugo kutoka chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali na wamesajiliwa na Bodi ya  Madaktari wa Mifugo Tanzania.

(b)               Majukumu
·        Kutoa  huduma za Afya ya Mifugo
·        Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo la sehemu alipo.
·        Kutayarisha  na kusimamia mipango ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
·        Kushiriki katika uchunguzi wa magonjwa ya wanyama pori katika eneo lake.

(c)                Mshahara
Mishahara ya watumishi wa Serikali ya TGS. F

5.Afisa  Utafiti Mifugo daraja la II (Livestock Research Officer II) (Nafasi 10)

(g)               Sifa za waombaji

Wawe wamehitimu Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
           
(h)               Majukumu
·        Kujifunza  na kumudu mbinu na taratibu za Utafiti wa Mifugo/Ndorobo
·        Kufanya utafiti chini ya usimamizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi.
·        Kuandika  na kuweka kumbukumbu za utafiti
·        Kusaidia  kuendesha Semina na Maonyesho ya Ufugaji bora
·        Kuandaa  mapendekezo ya Utafiti (Research Proposals) kwa kushirikiana na Afisa Utafiti Mifugo anayemsimamia.
·        Kufanya kazi zote kama atakavyoelekezwa na Mkuu wake wa kazi.

(i)                 Mshahara
Mishahara ya watumishi wa Serikali ngazi ya TGRS A

6.Daktari Utafiti Mifugo daraja la II (Veterinary Research Officer) (Nafasi 5)

(j)                 Sifa za waombaji
Wawe wamehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Sayansi ya tiba ya mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya madaktari wa Mifugo Tanzania.

(k)               Majukumu
·        Kujifunza na kumudu mbinu na taratibu za Utafiti wa Afya na Maradhi ya Mifugo.
·        Kuweka kumbukumbu za Utafiti
·        Kusaidia kuendesha Semina na Maonyesho ya Ufugaji bora
·        Kuandaa mapendekezo ya Utafiti (Research Proposals)  kwa kushirikiana na Daktari  Utafiti Mifugo anayemsimamia.
·        Kufanya  utafiti chini ya usimamizi wa Daktari Utafiti Mwandamizi
·        Kukusanya na kuchambua takwimu za Utafiti unaoendelea
·        Kuchapisha taarifa na makala za Utafiti
·        Kufanya kazi nyingine zozote kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

(l)                 Mshahara
Mshahara wa watumishi wa Serikali ngazi ya TGRS C.

MAMBO YA KUZINGATIA

Barua za maombi ziambatane na ‘Curriculum Vitae’ (CV), picha ndogo 2 ukubwa wa pasipoti, cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu elimu ya Sekondari na Shahada.

Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45

Wahitimu walioajiriwa Serikalini hawaruhusiwi  kuomba nafasi hizi kwa sababu tayari wana ajira.

Wahitimu waliotuma maombi yao kabla ya tangazo hili wanashauriwa kutuma maombi upya.

Barua  zote za maombi ziwasilishwe katika muda wa siku 21 kuanzia tarehe ya kwanza ya  kuonekana tangazo hili.

Barua za maombi zitumwe kwa:


Katibu Mkuu,
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,
S.L.P. 9152,
DAR ES SALAAM.


WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA UVUVI

(TAFIKO)

Wadai katika maombi Na. 73/2009 yalioko Mahakama Kuu mbele ya Mh. Jaji Mwarija wana nia ya kuendesha shauri lao kwa njia ya uwakilishi.Wanne kati ya wadai (JOHN KABUCHE, ROBERT KASIGA, SEIF MTUNYUNGU NA HADUA ABDALLAH) Wamejito0keza kuwakilisha wenzaowapatao 78 waliokuwa wafanyakazi wa shirika la uvuvi(Tanzania Fisheries Corperation).

Taratibu za kisheria zinahitaji ridhaa ya wadai wote kuhusu uwakilishi huo ili waweze kuteuliwa rasmi Mahakama.
 Madhumuni ya tangazo hili ni kuwataarifu wahusika wote (ambao wameorodheshwa hapo chini) ili muhusika yeyote mwenye pingamizi awasilishe pingamizi lake kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya tangazo hili.

JOHN KABUCHE
Kiongozi wa Wawakilishi.

WADAU KATIKA KESI.

  1. JOSEPH KAGUMILA
  2. DEUSDEDIT MAKARANGA
  3. JOSEPH MAPUNDA
  4. SALUM MWAGO
  5. ALLY ATHUMANI
  6. MBARAKA BARAKA
  7. ALPHONCE KWENDAKWENE
  8. SHIDA KILAGANE
  9. CATHERINE SHEMAKAME
  10. PROTAS MKUMBAE
  11. PATRICK HENDRY
  12. ALEXANDRE MASONDARE
  13. VERONICA MUGISA
  14. YUSUPH TINDWA
  15. PETER LUCAS
  16. BARICK MASAMU
  17. ALLY MACHEMBA
  18. OTICK MANGULA
  19. MODESTA FUNDI
  20. MOHAMED KIBAHA
  21. PATRICK NDONDE
  22. MARY MKUDE
  23. ALLY KIZITO
  24. SHABANI MGONJA
  25. THERESIA LUPOGO
  26. VIOLET CHIKUNI
  27. MOHAMED MUBA
  28. REMIX MASSENGE
  29. SAID NJENGE
  30. JOACHIM NYIMBI
  31. BENARD LUANDA
  32. DAMAS KAYANDA
  33. LEAH MGHENI
  34. JANE MASANJA
  35. NICODEMUS MANYAHI
  36. ELIA MLAY
  37. ABDALLAH NDALAMAH
  38. CHRISTOPHER MOREMI
  39. HUSNA MTORO
  40. FRANCIS R. NKOKA
  41. MOHAMED JUMBE
  42. HARUB HASSAN
  43. AWETU ABDALLAH
  44. AGREY MASANGANO
  45. ESAU MAPUNDA
  46. ABDUL KHATIBU
  47. MARTIN SIMON
  48. REVOCATUS ALEXANDER
  49. ESNATH SAMBO
  50. ALLY ABDALLAH
  51. ABDUL JUMBE
  52. LAWRENCE MABOSHO
  53. FESTO AMOS
  54. ELIZABETH MAGONGO
  55. EDSON E. BITEBO
  56. GIDEONI LIHULUKU
  57. HAJI IBRAHIM
  58. GRADY CHALUBE
  59. FRANCIS NINDI
  60. COSMAS SHIGANZA
  61. SHABANI AMOUR
  62. SHABANI SELEMANI
  63. YUSUPH ABDULRAHMAN
  64. JUMA O. YUSUPH
  65. ARCHARD ALOHONCE
  66. NICOLAUS CHIGAVA
  67. USHU OMARY
  68. MAGESA CHIBUGA
  69. RAMADHANI JUMA
  70. MOHAMED JORO
  71. RAMADHANI MPWITTO
  72. ISSA CHIPILAH
  73. EBEBEZA SWAI
  74. APRUNA HUMBA
  75. O.H MWANGA
  76. YUSTA ZAKAYO
  77. ABDU MASANGA
  78. YUSUPH ABDALLAH.

MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI IMEWAHI KUWA NA MAWAZIRI WAFUTAO KWENYE VIPINDI TOFAUTI NA WIZARA TOFAUTI TOFAUTI KAMA IFUATAVYO














SIKU YA UVUVI DUNIANI INAADHIMISHWA KILA MWAKA TAREHE 21/NOVEMBA YA KILA MWAKA

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi inapenda kuwajulisha Maadhimisho ya hayo yataadhimishwa rasmi kwa kuhusisha Wizara sehemu itakayofanyika kitaifa mtajulishwa baadaye .
Wizara itashiriki na inaomba wadau wote wa Sekta ya  Uvuvi kujiandaa kwa maadhimisho hayo ambayo mtanufaika na mambo mbalimbali yatakayoonyeshwa na kupata maelezo na taratibu mbalimbali katika kufanikisha biashara zako, pamoja tukishirikiana tutaondoa umasikini wa wananchi walio wengi

MDAU KUMBUKA MAADHIMISHO HAYA YANADHIMISHWA KAMA SEHEMU YA  MIAKA HAMSINI YA UHURU WA TANZANIA BARA.

WOTE MNAKARIBISHWA.