Nav bar

Jumamosi, 4 Juni 2011

SHEREHE ZA WIKI YA MAZIWA MKOA WA DAR-ES-SALAAM

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Benedict Ole Nangoro  alipohojiwa na vyombo mbalimbali vya Habari Siku ya Kilele cha Uhamasishaji Unywaji wa Maziwa Tarehe 31/05/2011 ndani ya Banda la Kampuni ya DESA ambao nao warishiriki katika kuonyesha bidhaa mbalimbali zitokanazo na Maziwa. 
Moja ya Viongozi wa Mkoa wa Dar-es-salaam alipotembelea Banda la Kinamama wa Kikundi cha Nronga kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai ambao nao wanazalisha bidhaa bora kabisa zitokanazo na maziwa.

Watoto waliotembelea banda ya TAMPRODA na kuweza kula bidhaa iliyotokana na maziwa kama wanavyooonekana kwenye  picha, anayewahamasisha kula ni Mjumbe Mama Mellewas viwanja vya Biafra Kinondoni Dar-es-salaam. 

Muonyeshaji wa shughuli zinnazofanywa na Bodi ya Maziwa Tanzania akimkabidhi Mhe Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,  moja ya vielelezo vya Bodi hiyo katika viwanja vya Biafra alipotembelea  mabanda ya bidhaa zitokanazo na maziwa siku ya Kilele cha Wiki ya Uhamasishaji Unywaji Maziwa.

Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, akimkabidhi Ndugu Nasinyari wa Kikundi cha Engtengi cha Wilaya ya Simanjiro, zawadi ya gold na silver ikiwa ni ishara ya uzalishaji wa bidhaa bora za kusindika  za Maziwa. Siku ya Kilele cha Wiki ya Uhamasishaji Unywaji Maziwa Kitaifa, Viwanja vya Biafra 31//05/2011
Dar-es-salaam. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi  Mhe. Benedict Ole Nangoro akihutubia Kilele cha Wiki ya Uhamasishaji Unywaji Maziwa Kitaifa uiliofanyika Dar-es salaam   katika viwanja vya Biafra Wilaya ya Kinondoni Tarehe 31/05/2011

Mhe Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Benedict Ole Nangoro akimkabidhi Mtotot wa Shule ya Msingi Msisiri  iliyopo Wilaya ya Kinondoni zawadi , baada ya kuwa washindi wa Nginjera bora katika Kilele cha Wiki ya Uhamasishaji Unywaji Maziwa .


Watoto wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Kinondoni,  wakifurahia kunywa maziwa Siku ya Kilele cha Wiki ya Uhamasishaji Unywaji wa Maziwa uliofanyika Kitaifa Mkoa wa Dar-es-salaam Tarehe 31/05/2011 katika viwanja vya Biafra Wilaya ya Kinondoni. 

Waziri wa Mendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David (MB) akiwa katika  picha ya pamoja na Uongozi wa Shirika la Ranchi za Taifa  (NARCO)