TASFAM YATAJWA KUONGEZA WIGO, KUKUZA SEKTA YA UVUVI
Na. Edward Kondela Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema uvuvi wa bahari kuu, ukuzaji viumbe maji, mafunzo na utafiti ni mambo muhimu katika kukuza Sekta ya Uvuvi nchini. Mhe. Balozi Dkt. Kakurwa amebainisha hayo leo (05.11.2026) jijini Dodoma, alipokutana na watekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usimamizi Endelevu wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), kutoka katika taasisi na idara zinazoshughulika na Sekta ya Uvuvi zilizopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Amesema mafunzo na utafiti yanaenda sambamba na uwepo wa maabara yenye ubora na usalama kwa ajili ya sampuli za bidhaa za uvuvi ili kuleta matokeo chanya. Ameongeza kuwa ni muhimu kutatua kwa haraka changamoto zozote zitakazokuwa zinajitokeza ili kutochelewesha baadhi ya shughuli katika utekelezaji wa mradi. Awali kwenye kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Sheikh, amesema atahakikisha mradi wa TASFAM, unaleta matokeo chanya yaliyokusudiwa, kati...