Na. Daudi Nyingo – Iringa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede, ameongoza zoezi la utambuzi na uchanjaji wa mifugo mkoani Iringa, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji Chanjo na Utambuzi wa Mifugo iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa mkoani Simiyu hivi karibuni. Akizungumza Julai 3, 2025, mkoani Iringa, Dkt. Mhede alisema kuwa kampeni hiyo ya miaka mitano inalenga kuchanja mifugo yote nchini kama sehemu ya uwekezaji katika sekta ya mifugo, unaowaletea faida wafugaji na kukuza uchumi wa taifa. “Tunalenga kuchanja ng’ombe wapatao 400,000 hapa Iringa. Tayari tumejiridhisha kuwa chanjo zipo za kutosha, na tumeanza kutembelea maeneo mbalimbali kama Kalenga na shamba la mifugo la Kibete, linalomilikiwa na Richard Philips, kuhakikisha zoezi linaenda vizuri,” alisema Dkt. Mhede. Mbali na ng’ombe, Dkt. Mhede alibainisha kuwa chanjo pia zitatolewa kwa kuku, na aliwahimiza wananchi ...
Maoni
Chapisha Maoni