◼️Yanyakua kombe na medali 2
◼️Yaingia kwenye orodha ya timu 5 bora za muda wote kwenye mchezo wa kuvuta kamba
◼️Yaacha historia ya kuwa timu yenye ushindani kwenye michuano ya SHIMIWI
Timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi imehitimisha michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali nchini (SHIMIWI) iliyokuwa ikifanyika kwenye viwanja mbalimbali jijini Mwanza kwa kishindo baada ya kufanikiwa kunyakua kombe moja na medali mbili kwenye michezo waliyocheza wakati wote wa michuano hiyo.
Timu hiyo imefanikiwa kubeba kombe moja la mchezo wa bao upande wa wanawake ambapo mchezaji Jamila Kalambo alinyakua ubingwa wa mchezo huo baada ya kumshinda Laina Abbas kutoka Wizara ya Maji.
Aidha timu hiyo imefanikiwa kupepea vema bendera ya Wizara yao baada ya kuibuka washindi wa 2 na 3 upande wa mchezo wa kurusha TUFE wanawake na wanaume na kufanikiwa kubeba medali 2 katika mchezo huo.
Katika hatua nyingine Wizara hiyo imefanikiwa kushika nafasi ya 4 kwenye mchezo wa kuvuta kamba (wanaume) huku timu hiyo ikitajwa kama timu yenye ushindani wakati wote wa michuano hiyo baada ya kufanya hivyo pia katika misimu miwili iliyopita.
Michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka imehitimishwa rasmi leo Septemba 16,2025 ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeahidi kurejea imara zaidi kwenye michuano ijayo.








Hakuna maoni:
Chapisha Maoni