◼️Watetea ubingwa wao kwa mara ya pili mfululizo
Mchezaji Jamila Kalambo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ameibuka bingwa wa mchezo wa bao baada ya kuibuka mshindi wa raundi zote kwenye michuano ya SHIMIWI inayoendelea jijini Mwanza.
Mchezaji huyo ambaye umahiri wake ulionekana mapema wakati wa kuanza kwa mchezo huo uliochezwa kwenye viunga vya CCM Kirumba, aliibuka na ubingwa huo kwa kuwashinda wapinzani wake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, TSC, RAS Arusha na RAS Geita ambapo aliibuka na alama 10 na kufuzu hatua ya robo fainali kabla ya kushinda hatua hiyo na nusu fainali na kufanikiwa kucheza hatua ya fainali dhidi ya mchezaji Laina Abbas wa Wizara ya Maji.
Mbali na ubingwa huo,Timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi mpaka sasa imefanikiwa kuwa miongoni mwa timu zenye mafanikio makubwa kwenye michuano ya SHIMIWI mwaka huu baada ya kuibuka mshindi wa 4 mchezo wa kuvuta kamba (Wanaume), mchezaji Theodata Salema kuibuka mshindi wa 2 na Afred Mushi kushika nafasi ya 3 kwenye mchezo wa kurusha TUFE wanawake na Wanaume.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni