Nav bar

Jumanne, 10 Mei 2022

MENEJIMENTI YA SEKTA YA MIFUGO YATEMBELEA MACHINJIO YA DODOMA KUKAGUA MAENDELEO YAKE

 


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina, akifafanua mambo mbalimbali juu ya kampuni iliyowekeza katika eneo la machinjio ya Mkoa wa Dodoma, mara baada ya kufika katika machinjio hayo akiambatana na viongozi wengine wa menejimenti  Sekta ya Mifugo. (30.04.2022)


Kaimu Meneja wa machinjio ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Kristian Mapunda (kulia), akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina akiwa ameambatana na viongozi wengine (hawapo pichani) wa menejimenti ya Sekta ya Mifugo, kwa ajili ya kupata taarifa ya utendaji kazi wa machinjio hayo pamoja na taarifa ya mwekezaji Kampuni ya ALKAFIL ambayo iliwekeza katika eneo la machinjio hayo kwa ajili ya kuchakata nyama na kuuza nje ya nchi. (30.04.2022)


Kaimu Meneja wa Machinjio ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Kristian Mapunda (kushoto) akizungumza na menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) iliyofika katika machinjio hayo. (30.04.2022)


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina (wa tatu) akiwa na viongozi wengine kutoka menejimenti ya Sekta ya Mifugo, kukagua eneo la machinjio ya Mkoa wa Dodoma lililovamiwa na wananchi na kufanya shughuli za kilimo bila kuwasiliana na uongozi wa machinjio na kuagiza taratibu zifanyike ili wananchi hao watambuliwe na kupewa utaratibu. (30.04.2022)


Viongozi wa menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), wakiangalia jengo la machinjio ya Mkoa wa Dodoma, mara baada ya kufika katika machinjio hayo ili kupata taarifa ya utendaji kazi wake pamoja na kampuni ya ALKAFIL iliyowekeza katika eneo la machinjio kwa ajili ya kuchakata na kuuza nyama nje ya nchi. (30.04.2022)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni