Na. Hamis Hussein
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Edwin Mhede amehitimisha mkutano wa wadau wa tasnia ya kuku ujulikanao (National Poultry Delivery Lab), uliofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Julai 16, 2025 katika hafla ya kufunga Mkutano huo Dkt. Mhede amesisitiza kuundwa haraka kwa kamati ndogo ya kiufundi itakayoratibu na kufuatilia maazimio ya mkutano huo na kuahidi kushirikiana nayo ili kuhakikisha kuwa Wizara kwa kushirikiana na wadau, inakamilisha na kuzindua Mkakati wa Tasnia ya Kuku.
Aidha, Dkt. Mhede amewapongeza wadau wa tasnia ya kuku walivyobainisha na kujadili changamoto na fursa za tasnia hiyo na kutoa mikakati ya kuinua tasnia hiyo , ikiwa ni hatua muhimu ya kuanisha masuala ya kuzingatia katika uandaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Tasnia ya Kuku Nchini.
Katika hatua nyingine Dkt. Mhede amesisitiza kuongeza wigo wa ushiriki wa wadau wengine katika mnyororo wa thamani ili kuhakikisha masuala yote ya kimkakati yanaingia katika mapendekezo hayo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni