Na. Hamis Hussein
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede amefungua Mkutano wa tasnia ya Kuku (National Poultry Delivery Lab) unaofanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar-es-salaam kuanzia leo Julai 15-16, 2025.
Mkutano huo umelenga kuwakutanisha wadau wa tasnia ya kuku ili kuchambua, kujadili na kutoa suluhisho ya namna ya kukabiliana na changamoto zinazopunguza ufanisi na ushindani wa tasnia ya Kuku nchini.
Akifungua Mkutano huo, Dkt. Mhede alielezea kuwa tasnia ya kuku imeajiri asilimia 65 ya vijana na asilimia 51 ya wanawake nchini
"Tasnia ya Kuku inachagiza ukuaji wa sekta nyingine ikiwemo Kilimo kutokana na mahitaji makubwa ya vyakula vya Kuku vinavyotokana na mahindi na soya ambayo vimeifanya tasnia hii ya kuku kuwa ya kimkakati nchini" alisema Dkt. Mhede.
Aidha, Dkt Mhede amewahimiza Washiriki wa mkutano huo kutumia jukwaa hilo kuchambua na kuanisha maeneo ya kimkakati ambayo yatatatua changamoto zinazoikabili tasnia hiyo pamoja na kujenga uwezo kwa wafugaji na wafanyabiashara wa tasnia ya kuku ndani ya nchi ili waweze kuzalisha kwa tija na kuyafikia masoko.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni