Nav bar

Jumatano, 15 Julai 2020

MAONYESHO YA 44 YA KIMATAIFA YA BIASHARA "SABASABA" 2020


Mgeni rasmi, Waziri wa Biashara na Viwanda, Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali akitoa hotuba katika hafla ya kufunga Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (sabasaba) iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (13.07.2020)Waziri wa Biashara na Viwanda kutoka Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waliokuwa meza kuu katika hafla ya kufunga Maonesho ya 44 ya kimataifa ya biashara (sabasaba) iliyofanyika. Wa kwanza kulia waliosimama ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari, Tanzania, ambaye pia alikuwa Muwakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Furaha Mramba. (13.07.2020)Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari, Dkt. Furaha Mramba akishiriki kuimba Wimbo wa Taifa muda mfupi baada ya mgeni rasmi kuwasili katika hafla ya kufunga Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (sabasaba) kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (13.07.2020)Mkuu wa Utawala JKT, Col. Julius Kadawi (kushoto) akieleza jambo alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (sabasaba) yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia anayemsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani (WMUV), Bezia Rwongezibwa. (13.07.2020)Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI), Dkt. Ismael Kimirei alikuwa ni miongoni mwa Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya kufunga Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (sabasaba) kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (13.07.2020)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni