Nav bar

Jumapili, 19 Julai 2020

DKT. NANDONDE ATEMBELEA KIWANDA CHA MOTHER DAIRIES LIMITED


Mkurugenzi wa uzalishaji na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Felix Nandonde jana alitembelea kiwanda cha kusindika maziwa cha Mother Dairies Limited kilichopo Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo ya kikazi Meneja wa uzalishaji wa kiwanda hicho Bw. Alle Makene alimweleza Dkt. Nandonde kuwa kiwanda kina uwezo wa kusindika lita za maziwa 5000 kwa siku na sasa kinasindika lita 2000 kwa siku sawa na asilimia 40 ya uwezo wa kiwanda hicho.

Kituo kinakusanya maziwa kutoka kwa wafugaji kupitia vituo vitatu (Milk collection centres) ambapo kiwanda kinanunua maziwa kwa bei ya shilingi 900 kwa lita moja kutoka kwa wafugaji.

Kiwanda cha Mother Dairies Limited kinatengeneza maziwa fresh na mtindi ambayo huuzwa katika masoko ya mikoa ya Lindi, Dar es Salaam na Pwani.

Kiwanda hicho kina utaratibu wa kuuza maziwa kabla ya kuwekwa kwenye vifungashio (bulk sale) kwa bei ya shilingi 1200 kwa lita moja ya maziwa fresh na shilingi 1300 kwa maziwa ya mtindi.

Aidha, Bw. Makene alieleza kuwa changamoto za tasnia ya maziwa ni pamoja na;
I. Upatikanaji wa maji baada ya mfumo wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuharibika tangu Mwezi Machi, Mwaka 2020 na;
II. Ubovu wa miundombinu ya barabara



Picha ya pamoja ya uongozi wa kiwanda cha kusindika maziwa Mother Dairies Limited ukiwa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, Bw. Gabriel Bura (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Dkt. Felix Nandonde wote kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi mara baada ya kufanya ziara ya siku moja katika kiwanda hicho kilichopo wilaya ya Rufiji mkoani Pwani baada ya kukagua uzalishaji wa bidhaa ya maziwa. (16.07.2020)



Kipimo kinachotumika kukagua ubora wa maziwa kabla ya kusindikwa katika kiwanda cha Mother Dairies Limited kilichopo wilaya ya Rufuji mkoani Pwani. (16.07.2020)

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Felix Nandonde (wa kwanza kushoto) akipata maelezo ya namna kiwanda cha kusindika maziwa cha Mother Dairies kinavyofanya kazi kutoka kwa meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Bw. Alle Makene. (16.07.2020)


Sehemu ya vifungashio vya maziwa vinavyotumiwa na kiwanda cha kusindika maziwa cha Mother Dairies kilichopo Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani. (16.07.2020)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni