Nav bar

Jumatatu, 27 Julai 2015

ROMWALD SHEMKAI ALIEKUWA AFISA UVUVI HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO MKOA WA GEITA AFARIKI DUNIA JANA ASUBUHI TAREHE 26/07/2015 KWA AJALI YA PIKIPIKI AKITOKEA MUGANZA KWENDA CHATO.

Bw. Romwald Shemkai aliekuwa Afisa Uvuvi Halmashauri ya Chato Mkoa wa Geita afariki dunia jana asubuhi tarehe 26/07/2015 kwa ajali ya pikipiki akitokea Muganza kwenda Chato. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.

Jumatatu, 20 Julai 2015

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA MRADI WA LIVESTOCK MODERNIZATION INITIATIVE




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza kwa Makini Muendesha Mada ya Livestock Modenization Initiative Dkt. Kaush Arha  (hayupo pichani) Kama Utangulizi kabla ya Kuzindua Mpango huo katika Hoteli ya Kilimanjaro Jijini Dar-Es-Salaam

Dkt Kaush Arha wakati akitoa Maelezo ya Utangulizi ya Mpango Kabambe wa Jitihada za Kuboresha Sekta ya Mifugo (Livestock Modenization initiative) muda mfupi kabla ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baadhi ya Washiriki wa Mpango Kabambe wa Jitihada za Kuboresha Sekta ya Mifugo (Livestock Modenization initiative) Wakimsikilisha Muongoza Mada akitoa utangulizi wa Mpango huo.(hayupo pichani)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba Akisoma Hotuba kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Titus Mlengeya Kamani  kabla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) akifatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Kapteni Mstaafu Chiku Ghalawa kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa yenye Mifgo Mingi Tanzania (mwenye kilemba) wakifatilia kwa Makini Hotuba ya Waziri iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Mkuu wa Wizara (hayupo pichani)  

Baadhi ya Washiriki wa Mpango Kabambe wa Jitihada za Kuboresha Sekta ya Mifugo (Livestock Modenization initiative) Wakimsikilisha Muongoza Mada akitoa utangulizi wa Mpango huo.(hayupo pichani)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Akitoa Hotuba kabla ya Kuzindua Mpango Kabambe wa Jitihada za Kuboresha Sekta ya Mifugo (Livestock Modenization initiative) katika Hoteli ya Kilimanjaro Tarehe 20/07/2015



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Akiangalia Kitabu ambacho anatakiwa kukizindua ili Asaini . Waliomzunguka ni Mabalozi, Wakuu wa Mikoa na Sekretariet ya  Mpango Kabambe wa Jitihada za Kuboresha Sekta ya Mifugo 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Akisaini Kitabu cha Mpango Kabambe wa  Jitihada za Kuboresha Sekta ya Mifugo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Wadau wa Sekta ya Mifugo nje ya Ukumbi wa Hoteli ya Kilimanjaro

Baadhi ya Washiriki wa Mpango Kabambe wa Jitihada za Kuboresha Sekta ya Mifugo (Livestock Modenization initiative) Wakimsikilisha Muongoza Mada akitoa utangulizi wa Mpango huo.(hayupo pichani)








                                









Alhamisi, 9 Julai 2015

KATIBU MKUU WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI DKT. YOHANA BUDEBA AFANYA MKUTANO NA WATUMISHI WA FETA (WAKALA WA MAFUNZO YA ELIMU YA UVUVI ILIYOFANYIKA MBEGANI - BAGAMOYO

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba  kushoto Bi. Tabu Chando Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu akifatana na Mtendaji Mkuu wa FETA Bw. Yahaya Mgawe kushoto ni Bw. Mashaka Shabani Afisa Kilimo II pamoja na Bw. ZK Makame Afisa Tawala Mkuu wakiangalia bwawa lenye vifaranga vya samaki 
Moja kati ya bwawa la vifaranga vya samaki wa aina mbalimbali katika eneo la Mbegani Bagamoyo
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba akiangalia moja kati ya bwawa la vifaranga vya samaki aina ya kambare jinsi  wanavyofugwa kulia ni Bi. Tabu Chando Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu akifuatana Bw. Mashaka Shabani Afisa Kilimo II Idara ya Viumbe kwenye maji  kushoto ni Bw. Abdul Kashaija Pamoja Bw. ZK Makame Afisa Tawala pamoja na Mkuu Mtendaji Mkuu wa FETA Bw. Yahaya Mgawe 


Bw. Mashaka Shabani Afisa Kilimo  Idara ya Viumbe kwenye maji akimuelezea Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba uzalishwaji wa vifaranga vya samaki hao
Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba  na Bi. Tabu Chando Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wakiwa na baadhi ya watumishi wakiangalia bwawa kubwa la samaki

Mmoja wa wafanyakazi Idara ya Viumbe kwenye maji Bw. Abdul Kahaija akionyesha jinsi ya  ulishwaji wa samaki hao

Maboti ya kuvulia samaki yakiwa yametia nanga


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba na Bi. Tabu Chando Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wakimsikilza kwa makini Mtendaji Mkuu wa FETA akiwasilisha taarifa yake (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi. Tabu chando akiwaeleza wafanyakazi taratibu Sheria na kanuni za kiutumishi Serikalini
Bw. Godifrey Christopher kutoka Idara ya Ubaharia na Uvuvi (FETA) akitaka kujua sera ya kuajiri kwa Watumishi
Bw. Walilo Yasin Teknolojia wa Samaki (FETA) akiuliza kuhusiana na maslahi ya Mtumishi akiumia kazini

 Bi.  Emakulata Ndalawa kutoka Idara ya Ubaharia na Uvuvi akimshauri Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba  "Mkiuza Meli Mnunue Meli"
Moja kati ya boti kubwa linalotengenezwa kwa ajili ya kuvulia samaki Bahari kuu (Deep Sea)
Mazingira mazuri  ya Mbegani Bagamoyo

Bw. Mashaka Shabani  Afisa Kilimo II Kutoka Idara  ya Viumbe kwenye Maji atoa wazo juu ya Ununuzi wa Mashine ya kuzalishia chakula cha samaki
Bw.  Tukaye Mngonji akiuliza kuhusu utaratibu wa uchangiaji wa bima ya afya serikalini 
Bw. Juma Mkumba akitaka ufafanuzi juu ya  Watumishi wa Umma kukaa sehemu moja kwa muda mrefu katika vituo vyao vya kazi
Bw. Emmanuel Mboge Mhasibu wa FETA akiuliza swala la kupandishwa cheo 

Ijumaa, 3 Julai 2015

ZIARA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI DKT. TITUS KAMANI ILIYOFANYIKA WILAYANI KITETO MKOA WA MANYARA NA KILINDI - TANGA KWA MADHUMUNI YA KUKAGUA UJENZI WA MABWAWA YA MAJI

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara
Mkurugenzi wa Ugavi na Ununuzi Bw.Gaston Lugali akifafanua jambo linalohusiana na ujenzi wa bwawa la Kiteto katika kijiji cha OLPOPONG
Bwawa la Maji katika Kijiji cha Olpopong lililochimbwa na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Wafugaji wa Kiteto wakisikiliza kwa makini hotuba inayotolewa na Mhe. Waziri (hayupo pichani)
Pembezoni mwa bwawa la Maji
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Bi. Anuciata Njombe akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa bwawa (hayupo pichani)

Mhe. Waziri Dkt. Titus Kamani akisalimiana na wafugaji wa Wilaya ya Kiteto

Picha ya pamoja ya Mhe. Waziri Dkt. Titus Kamani kulia Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kanali Nzoka anaefata ni Mkurugenzi wa Ugavi na Ununuzi Bw. Gaston Lugali pamoja na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Bi. Anuciata Njombe  Wakiwa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Kiteto

Mandhari ya Wilaya ya Kilindi
Mhe Waziri Dkt. Titus Kamani akisalimiana na kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kilindi

Waziri akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilindi

Mhe Waziri Dkt. Titus Kamani akimsikiliza Mbunge wa Kilindi Mhe. Bi Beatrice Shelukindo wakati akiongea na wananchi wa kijiji cha Wialayani Kilindi

Mitambo ya uchimbaji wa bwawa la Kwamaligwa likiwa kazini
Eneo ambayo bwawa la Kamwaligwa litajengwa